MBINU
ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
- Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni
Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi
aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1.
Kusikiliza 2.kuzungumza 3. Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha
ile
Malengo
ya jumla ya kufundisha ili ni pamoja na:-
1)
Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.
2)
Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika
LUGHA YA KWANZA
Stern (1983) anasema kwamba “lugha
ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama yake mzazi angali mchanga.
LUGHA
YA PILI
Stern (1983) anasema kwamba “ lugha
ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza kukua na kupata lugha. Hii
ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari ana lugha
nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi
LUGHA
YA KIGENI
Ni ile lugha ambayo unajifunza na
kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au mbali na jamii anapokaa
mwanafunzi huyo. Mfn lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa Tanzania
MALENGO
YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI
Mara nyingi hii hutegemea taaasisi
yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla:
1)
Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika
2)
Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali
3) Kwa
ajili ya kufanya biashara
4)
Kukidhi vigezo vya masomo
5)
Kufanya utafiti katika taaluma husika
6) Ili
kupata ajira nchi za ng’ambo
KITU
GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?
Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo
kwanza, utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako
W Anza
na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha muhimu
sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.
MALENGO
YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI
a) Ili
mwanafunzi wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:
i.
Aweze kumudu lugha ya Kiswahili
ii.
Aweze kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili
iii.
Ili wanafunzi waweze kung’amua mambo yafuatayo:- Namna ya kusema jambo gani?
Mfano anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa nini aseme? Kwa nani aseme?
Mazingira gani aseme?
iv.
Ili kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya Kiswahili.
Wanafunzi wafanye kwa vitendo ili waweze kujichukulia misamiati ya kutosha
v.
Wanafunzi wang’amue umuhimu wa lugha wanayojifunza
b) ili
wanafunzi waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni lazima wape wanafunzi:
kuchunguza®kugundua®kutalii kuhusu
lugha ya Kiswahili
c)
wape uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza msamiati kwa
kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi
d) wape
nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa wao
e)
wape uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi
f)
wasaidie kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na utamaduni wa lugha ya
Kiswahili
NADHARIA
KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA
Kuna mambo mawili ambayo waalimu tarajili
wanapaswa kujua
1)
mbinu za kujifunza lugha ya pili ni nyingi kama ilivyo waalimu
wengi
2)
manzingira halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers (2001) anasema kwamba “
wakati wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya
kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao”
kuna nadharia kuu nne (4)za
ujifunzaji lugha:
1)
NADHARIA YA UHULKA
ü Mwasisi wake ni Noamy
Chomsky (1957)
ü Wazo kuu lake ni kwamba:
binadamu huzaliwa akiwa na uwezo lugha. Yaani kwenye ubongo wake ana mfumo
ambao huzaliwa nao kwa ajili ya kujifunza lugha. Ana kifaa kinachoitwa LAD
(Kifaa cha upataji lugha)
ü Naye Brown (2000) aliunga
mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga mkono ni Ellis (1997) walikuwa na hoja
kwamba kuna kipindi mtu akifikia umri Fulani hawezi kupata lugha sawasawa
na wazawa wa lugha husika. Umri huo ni kuanzia 0-miezi 18. Kwa mujibu
wa wataalamu hawa mazingira hayana msaada wowote katika ujifunzaji lugha.
2)
NADHARIA YA UTABIA
ü Kwa mara ya kwanza
ilidokezwa na E.Thonilke(1935). Kwa mujibu wa wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigo
ü Aliyetafiti zaidi katika
nadharia ya ujifunzaji ni B.F SKINNER , Huyu alikubali ni mwigo lakini
akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo mtoto mdogo hazaliwi na lugha
bali huichota kutoka kwa wazazi wake
- Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika
ujifunzaji lugha
- Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha? Jibu
unalo wewe mwenyewe!
3) NADHARIA
YA UTAMBUZI
ü Nadharia hii iliasisiwa na
Jean Hajet (1954)
ü Alidai kuwa binadamu
anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata lugha
ü Alidai kuwa kujifunza lugha
ni sehemu ya makuzi ya binadamu, kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyozidi kupata
lugha
ü Alidai kuwa mtoto hupata
lugha kabla ya kuzaliwa.
ü Arth(2003) anadai
kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa,kuanzia 0-miezi 18
ü Nadharia hii haipingani na
umuhimu wa mazingira katika ujifunzaji lugha
4)
NADHARIA YA UUMBAJI/ MAUMBILE
ü Iliasisiwa na Jerome Brunner
ü Wazo kuu la nadharia hii
inasisitiza nafasi ya mama katika upataji lugha ya kwanza
ü Mtoto hutengeneza lugha
kutegemeana na mawasiliano ambayo mama yake anayatumia
ü Alidai, ili mtoto aweze
kupata lugha ni lazima mambo yafuatayo yatimizwe
- Muktadha
- Tajiriba (experience)
- Upangilifu (organization)
- Kujenga mazingira ya upekuzi (udadisi_
ü Hukaza zaidi kuhusu
mazingira katika ujifunzaji lugha
NJIA
ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI
Njia za ufundishaji Kiswahili ni
nyingi kama na waalimu nao walivyo wengi, lakini njia hizi itatengemea hali ya
wanafunzi, hata hivyo njia zifutazo zinapendekezwa zitumike.
- Njia ya majadiliano-njia hii haifai kwa mwanafunzi
ambaye ndio kwa mara ya kwanza anasikia Kiswahili. Lakini ni njia nzuri
kwa mwanafunzi ambaye amewahi kusikia habari za Kiswahili
- Njia ya mahojiano. Mfano mwalimu aandae maswali,
awaambie wanafunzi wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa daktari mwingine
anakuwa mgonjwa n.k
- Mchezo wa maswali. Kwa mfano. Kama wewe ungekuwa rais
wa marekani ungefanyaje kuhakikisha unakomesha ugaidi duniani? Watajibu na
kujipatia msamiati kibao
- Njia ya uigizaji-mwli awape wanafunzi mwongozo wa
maigizo
- Njia ya maswali ya papo kwa papo (ana kwa ana) mfano:
mimi ni Seni, wewe ni nani?
- Njia ya uwandani. Mfno ukitaka kuwafundisha misamiati
ya sokoi wapeleke sokoni.
- Njia ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama
mwalimu anataka kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira
- Njia ya usomaji. Mfano kusoma pande nne za dunia,kuwapa
matini mbalimbali wanafunzi
- Njia ya majadiliano funge. Yaani wanafunzi wanajadili
vitu ambavyo vimewekewa mipaka
Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike itategemea aina ya wanafunzi na
kazi zao!
HULKA/TABIA
YA UANAFUNZI KUJIFUNZA LUGHA
Wanafunzi hutofautiana kulingana na
hulka zao, mwalimu anahitaji kuangalia mielekeo ya wanafunzi wake. Baadhi ya
tabia zao ni kama vile: ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua, hapendi
kusahihishwa, mkimya nk
ATHARI
ZA KIJAMII KUHUSU LUGHA/WANALUGHA
Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu
ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio ambao huathiri ujifunzaji lugha na
kupelekea kutopata motisha wa kujifunza lugha. Baadhi ya mambo yanayoathiri ni
kama vile
i.
Nia au lengo la kujifunza lugha hiyo
ii.
Jinsia
iii.
Umri
iv.
Mazingira
v.
Umilisi wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo
Malengo ya mwalimu ni kuhakikisha
anafanya mambo yafuatayo:
i.
Kuwatia motisha wa kujifunza lugha
ii.
Kumsaidia kuondokana na hasira
iii.
Kuondoa dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna wanaoamini kwamba Kiswahili
ni lugha ya kiislamu
iv.
Kuondoa utata katika vipengele vya kisarufi
v.
Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika
Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara
ni muhimu sana kujua ishara zinazotumika katika jamii. Hivyo mwalimu anapaswa
awaeleze mambo yafuatayo
i.
Baadhi ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini
ii.
Matumizi ya mkono wa kushoto au wa kulia
iii.
Kuonyesha vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa
iv.
Namna ya kusimama na kuelezea jambo
Ili kutimiza hayo yote mwaimu lazima
awe na sifa zifuatazo:
i.
Awe muwasilishaji mzuri
ii.
Awe na mpangilio mzuri
iii.
Awe mstahimilivu
iv.
Awe na ujuzi wa kufundisha
v.
Awe na uhusiano mzuri na wanafunzi
vi.
Awe na maarifa ya somo
SIFA ZA MJIFUNZAJI LUGHA
a) Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila
kulazimishwa
b) Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo
c) Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo
ambayo jamii Fulani inayafanya
d) Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo
e) Awe na ratiba ya kujifuza
f)
Aweze kulinganua na kulinganisha
lugha anayojifunza
g) Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika
h) Awe mtendaji
i)
Azingatie ubora ili aweze kujifunza
zaidi
MOTISHA
Ni tabia au msukumo katika kutimiza
malengo Fulani. TUKI (2004) wanadai kuwa motisha ni kitu kama fedha inayotolewa
ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.
Hata hivyo, si lazima umpe kitu bali
unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu anapaswa kutumia motisha chanya
sio hasi. Mfn hutakiwi kuchapa fimbo
Brown (1994) anasema kuwa motisha:
a) Ni
kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia
b)
Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo
SKINNER &WATTSON-hawa
wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na
kujenga hali Fulani
AINA
ZA MOTISHA
- Mwamko wa mjifunzaji mwanyewe
- Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano,
darasa, nje n.k
- Jamii inayomzunguka ni motisha pia
- Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
- Zana/vifaa vya kujifunzia pia ni motisha
- Motisha wa ndani-
MOTISHA
IPO KATIKA MAKUNDI MIWILI
ü Haitegemei vitu vya nje ya
yenyewe
ü Hiki ni kile kinachoonekana
kwa mjifunzaji lugha mwenyewe
ü Hii haibadiliki kulingana na
muktadha wowote ule
- Motisha wa nje
ü Ni aina ya motisha ambayo
mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona
ü Hivi vitamsaidia katika kujifunza
lugha
Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia
lugha kulingana na muktadha. Hapa kuna mambo ya kuzingatia:-
a) Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao katika akili
zao ili kujifunza lugha
b) Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza lugha
c) Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha
d) Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha haraka
kuliko wanaume
UFUNDISHAJI
LUGHA KIMAWASILIANO
ü Ni muhimu kuhakikisha kwamba
katika kujifunza lugha ufundishaji uwe wa mawasiliano
ü Ni mbinu ya kufundisha lugha
ngeni na lugha ya pili
ü Husisitiza mwingiliano
maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha
KAZI
ZA LUGHA
ü Van (1975) anasema
kuwa kazi ya lugha ni:
a)
Kutoa habari
- Kusimulia
- Kuuliza
- Kutoa taarifa
b)
Kutafuta taarifa za kitaaluma
c)
Kuelezea mihemuko na misisimko. Mfno mapenzi, misisimko
d) Kuelezea
masuala ya uadilifu.mfn kuomba msamaha, ibada etc
e)
Kwenye mambo ya ushirikiano. Mfn kuamkia watu, kujitambulisha nk
Angalizo: hata kama mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha
hiyo ni lazima umfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha
MASHARTI
YA KUZINGATIA
a)
Azingatie majukumu ya kijamii mfn ataanzaje kuzungumza na mtu asiyemjua? Watu
wengine ni wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna ya kuzungumza nao
b)
Majukumu ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfn CHADEMA CUF na CCM
c)
Mazingira ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu wanaokuzunguka
wanatumiaje?
Angalizo: lugha sio sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha
mawasiliano, hivyo inahitaji kufundishwa kimawasiliano zaidi
MUKTADHA
WA UFUNDISHAJI LUGHA
ü Haya ni mazingira halisi
ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika kwa kuzingatia wadau wakuu watatu
a)
Mwanafunzi
b)
Mwalimu
c)
Jamii
ü Pamoja na motisha
ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:
- Utoaji wa kazi na mazoezi mengi
- Tumia lugha katika mazingira halisi na yanayostahili
ukilenga kwenye stadi nne za lugha
- Matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha
- Utumizi wa mazingira halisi ya darasa.mfn picha,
katuni. Nk
- Himiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na
baina yako mwalimu
- Tumia mbinu zaidi ya moja. Mfn vikundi, majibizano nk
(rejea mbinu)
- Fafanua kwa uangalifu masuala ya kisarufi
- Ajue maono ya mwanafunzi. Mfn huzuni, ucheshi nk
- Kuunda mazingira ya utani darasani
UFUNDISHAJI
WA DARASA MSETO
ü TUKI (2013) Mseto ni hali ya
kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali kutengeneza kitu fulani
ü Hapa ni mchanganyiko wa
darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali na wenye umri tofauti,
malengo tofauti nk
ü Hivyo mwalimu inakubidi
utofautishe sana katika ufundishaji wako na uwe makini ili usije ukawakwaza
wanafunzi wengine
NAMNA
YA UFUNDISHAJI DARASA MSETO
a) Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfn utamaduni
wao. Kama ni wazungu, wachina nk jua utamaduni wao
b) Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni Kiswahili basi
pendelea kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na lugha
ambayo wewe unaijua
c) Tumia vitendo halisi, ishara nk
d) Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na
mazingira
e) Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi
f)
Ufundishaji wa masuala ya utamaduni
lazima ufungamane na muktadha husika
SIFA
ZA MPATAJI LUGHA
Mpataji lugha ni lazima awe na sifa
kuu mbili tu:
- Umilisi wa kiisimu
ü Ni uwezo alio nao mjifunzaji
lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo, miundo tofauti ya lugha na
msamiati wa lugha
ü pia kuweza kutamka lugha
ile.
- Umilisi wa kiisimujamii
ü Ni umilisi ambao mtumiaji wa
lugha hupata lugha inayomwezesha kujifunza lugha na kuzingatia muktadha
NADHARIA
/MBINU /MIKABALA ZA KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI
ü Nadharia ni mkondo wa mawazo
unaotumika kuelezea jambo
ü Mtesigwa(2009) anasema “
nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo vinavyohusisha uchunguzi,
mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala fulani kisayansi
®kuna mambo mawili ambayo lazima
tujikumbushe:
a)
Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo wengi
b)
Kumbuka hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani, usitumie njia
moja tu.
ü Rogers&Richards
(2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji kujiuliza
maswali yafuatayo:-
a)
Malengo ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao linaweza
kuwa wanataka kuzungumza tu.
b) Upi
ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfn kaida
za lugha ya Kiswahili ni zipi?
c) Ni
misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?
d) Ni
misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la utamaduni,
mfano salamu nk
e) Je
lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano miundo
ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?
f)
Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?
g) Je
ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili (kigeni)?
NADHARIA ZA KUJIFUNZA
- Mbinu ya tafsiri sauti
- Mbinu ya moja kwa moja(direct method
- Mbinu ya usomaji(reading approach method)
- Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
- Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
- Mbinu ya ukimya (silence method)
- Mbinu ya mawasiliano (communicative language approach)
- Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
- Mbinu ya utambuzi (communitive code method)
- Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
- Mbinu ya tafsiri sarufi
ü wakati mwingine hujulikana
kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni mkabala ambao ufundishaji wa lugha ya kigeni
umejiegemeza katika sarufi ya lugha ya Kiratini. Iliasisiwa/anzishwa na
Meidinger (1783) na Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba lugha ya
kiratini ndiyo lugha pekee.
ü Nafasi ya lugha mama
ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika sarufi ya Kiratini, na hivyo
mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha sarufi ya Kiratini na vipengele
vingine vilipuuzwa
ü Huu ulikuwa ni mkabala
elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya kutumia lugha na sivyo wanajamii
wanavyotumia lugha hiyo
- Mbinu ya moja kwa moja(direct method)
ü Iliasisiwa na Gouin(1880)
ü Nadharia hii inazingatia
uzungumzaji wa lugha husika
ü Mbinu zilizopaswa
kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi kuzungumza. Mfn mbinu ya
majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi
ü Masomo yalianza kwa hadithi
fupi halafu wanafunzi wanauliza maswali kuhusu hadithi waliyosimuliwa na
mwalimu aliwaambia watoe maoni yao kuhusu hadithi hiyo.
ü Matumizi ya vielelezo
vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k
ü Kipengele vya sarufi
kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi ambamo lugha inatumika
ü Kipengele cha utamaduni
kilifundishwa kwa uchache sana
- Mbinu ya usomaji (reading approach method)
ü Mbinu hii inatumika
kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni ambao hawatarajiwi
kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo inatumika
ü Malengo yake huwa kuendeleza
uwezo wao wa kusoma ile lugha
ü Vipengele vinavyofundishwa
ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo vipengele vingine havihusiki. Mkazo wake ni
kwamba anayejifunza lugha aweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.
ü Mbinu hii haimpi mjifunzaji
lugha uwezo wa kuzungumza lugha husika bali ni kuisoma tu.
- Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
ü Nadharia hii ilitokana na
haja ya ukarimani nchini marekani miaka 1940.
ü Iliasisiwa na Bloomfield
(1942) na Fries (1945)
ü Msingi mkubwa wa nadharia
hii ni kile kinachosemwa
ü Maandishi hayakupewa fursa
kubwa bali kile kilichosemwa ndicho kilikuwa cha muhimu sana. Bloomfield
alisema kuwa lugha si katika maandishi bali ni kile ambacho kinasemwa.
ü Inahusisha kusimulia mada
mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia
ü Walipenda sana kutumia
miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji
ü Walisisitiza stadi ya kusikiliza,
kuzungumza, kusoma na kuandika
ü Waliongeza kitu kingine cha
kuona
- Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
ü Iliasisiwa na curran
(1976)
ü Dai la nadharia hii ni lugha
ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi kutenga jamii na lugha
ü Walidai kwamba ili uweze
kumfundisha mwanafunzi mgeni basi nenda kwenye jamii husika
ü Walidai pia kwamba kama utaamua
kufundishia darasani bali darasa lako lifanye angalau lifanane fanane na jamii
ya lugha husika
ü Ili uweze kufundisha watu ni
lazima ushirikishe watu wanaotumia lugha hiyo.
ü Mwanafunzi atapata vichocheo
vya aina nyingi katika jamii na kubaini ni mambo gani yanafaa na mambo gani
hayafai
ü Nadharia hii inaipa
kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika kujifunza lugha
- Mbinu ya ukimya (silence method)
ü Nadharia hii inaamini kwamba
kila lugha ina mfumo wake tofauti na lugha nyingine, hivyo ufundishaji wa lugha
ya pili ulenge kumfanya mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi au kukaribia kuwa
mmilisi wa lugha anayojifunza
ü Nadharia hii inadai kwamba
ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha vitu viwili.
Kichocheo®
Mwitikio® mgeuko
(Mwalimu)
(mwanafunzi)-(anabadilika)
ü Ili kuweza kutimiza hili,
mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya utani katika darasa jambo ambalo
litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa lugha husika
ü Nadharia hii inamhitaji
mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi wake ili kubaini kama kuna badiliko
- MBINU YA UTAMBUZI (COMMUNITIVE CODE METHOD)
ü Nadharia hii inatokana na
ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya sarufi na ile ya moja kwa moja
ü Ilianzishwa mwaka 1970
ü Wanadai kwamba mwanafunzi
apewe vipengele vyote vya lugha kwa ujumla mwanafunzi kumpa maarifa mapana
kuhusu lugha, kumpakanuni za msingi kuhusu lugha, halafu yeye mwenyewe kulingana
na utambuzi wake aweze kuielewa lugha.
ü Uwafundishe kanunu za
msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili ni lazima ujue ngeli za majina-hii
itakusaidia kutumia nomino katika mazingira tofauti tofauti, vitenzi-waeleze
namna ambavyo vinaweza kukaa peke yake kama sentensi
- Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
ü Nadharia hii pia hujulikana
kama mkabala asilia.
ü Iliasisiwa na James na
Asher
ü Inatilia mkazo mfumo na
muundo wa lugha.
ü Kama ilivyo nadharia ya
usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu wa kumudu mazungumzo kama sehemu
ya umilisi wa lugha
ü Ufundishaji uhusishe mazoezi
ya kurudia rudia ambayo angalau unamfanya mwanafunzi kumudu anachojifunza
ü Nadharia hii inasisitiza
matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali kama nyenzo mojawapo katika kujifunza
lugha.
- Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
ü Ilianzishwa na Lonzano
georgi (1979)
ü Nadharia hii inayapa
mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo muhimu mojawapo katika kujifunza
lugha. Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayotumika kujifunzia lugha ni lazima
yamkumbushe mwanafunzi kile alichojifunza jana yake
ü Wanaelezea namna ya mkao
wakati wa kufundisha wanafunzi wageni. Mkao katika darasa uwe ni wa kutazamana,
maana yake vikae kwa duara.
ü Wanasisitiza matumizi ya
mziki laini na mziki nyororo
-
MBINU YA MAWASILIANO (COMMUNICATIVE LANGUAGE APPROACH)
ü Inasisitiza maingiliano na
maathiriano katika ya mwalimu, mwanafunzi na jamii
ü Wanakaza kwamba kujifunza
lugha ni kujifunza kuwasiliana.
ü Kujua lugha kwa hakika sio
kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana na watu wa jamii
ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika
ü Ni nadharia ambayo
imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky
ü Hii ndiyo nadharia ambayo
inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza lugha
VIWANGO VYA WANAFUNZI
- Hapa inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha
Fulani.
- Viwango hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja
isiyokuwa ya kibiashara wala kiserikali liitwalo Interagence Language
Round Table (ILRT)
- Kulingana na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika
viwango vitatu
a)
Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
b)
Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)
Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
a)
Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
Daraja limegawanyika katika viwango
hivi
- Kiwango cha 0-®mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza
lugha
- Kiwango cha +0-®mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji
muhimu akibadilishiwa tu basi Amepotea
- Kiwango cha 1-®mwanafunzi anaweza kusitahimili
mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo
- Kiwango cha +1-®huyu anaweza kuanzisha mazungumzo yeye
mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi matarajio yake
INTERMIDIATE
- Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa
urahisi
- Kiwango cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo
sahihi, ana msamiati wa mazingira fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya
kitaaluma
- Anaweza kukithi mahitaji ya kitaaluma
b)
Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)
Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
Hakuna dhana ya lugha lengwa ikiwa Kama dhana ya msingi katika ujifunzaji na ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni
ReplyDeleteKivipi unaweza kufundisha lugha ya kigeni bila kuwa na mitaala
ReplyDelete