Monday 3 April 2017

lugha ya KISUKUMA

jina Wasukuma linatokana na neno “sukuma” lenye maana ya “kaskazini” katika lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi. Wanyamwezi waliwaita “Bhasukuma” yaani watu wa kaskazini mwao. Nao Wasukuma waliwaita Wanyamwezi “Bhadakama”.
Maria Nyanjige akinukuliwa, asema anafafanua kuhusu historia ya Wasukuma, “ kihistoria asili ya kabila la wasukuma ni nchini Ethiopia, na akaongeza kuwa kabila la Wasukuma limegawanyika katika sehemu tatu, kwamba kuna wasukuma wa Mwanza, Wasukuma wa Tabora na Wasukuma wa Shinyanga, akaeleza kuwa pamoja na kugawanyika kwa makabila hayo lakini bado yanalafudhi inayotofautiana kwa namna moja ama nyingine” kuna maelezo yahusuyo makumbusho ya Bujora ambapo tamaduni za Wasukuma zimehifadhiwa. Bujora zamani iliitwa Kujorwaningo kutokana na eneo hilo kuwa hatari kutokana na wanyama hatari na watu wanyongao watu wengine, hivyo eneo hilo likabatizwa jina la kujorwaningo yaani kwa kisukuma kunyonga shingo.
inaelezea kuwa Kisukuma ni lugha ya kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasukuma mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kisukuma imehesabiwa kuwa ni watu milioni 543000. Kufuatana na Uainishaji wa lugha za Kbantu wa Malcom Guthrie, Kisukuma iko katika kundi la F20. inafanana na lugha ya Kinyamwezi.
Jina  “Wasukuma” lina maana ya watu wa  “kaskazini” lakini maana hii haiwakilishi maana  halisi ambayo watu wengi huitafsili kwa mfano  Wasukuma  hutumia alama  ya utambulisho  kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila kwa  mfano jina  kama hili: Kiiya lina maana ya  mashariki ambako ni mawio ya jua.  Huu ni utambulisho ambao haukufanikishwa    ama kuitwa kwa jina  la kabila fulani mfano mwingine ni upande wa  “dakama”  ambapo yatambulisha  kama eneo la Unyamwezi lakini zaidi ya mpanuko wake  ni upande wa “kusini” zaidi ya hapo neno hili hutumiwa  sana  na kabila  la Wanyamwezi ili kutambulisha eneo la Wasukuma ambapo Wasukuma  nao husema  “dakama” upande  mwingine ambao unapewa alama  ya utambulisho wa neno “shashi” maana  yake  ni upande wa kabila  la “Washashi”  na neno hili washashi ni  mkusanyiko  wa makabila  ya mkoa  wa Mara.
Japo pia neno hili “shashi” linamaanisha kabila la Wakurya ambao pia mpanuko wake unakomea hapo ambapo zaidi ya eneo zima la upande huu unamaanisha upande wa kaskazini. Upande wa mwisho kutambulishwa   ni “Ngw’eli” neno hili  halikupewa kabla na  badala yake linamaanisha upande  mashariki (dira), ambako ni machweo ya jua. “Wasukuma  wenyewe hulirejelea jina hili kama “bhasukuma” kwa umoja “nsukuma”
Wasukuma huishi eneo  la kaskazini mashariki  mwa Tanzania, karibu  na  mwambao wa  kusini mwa  ziwa Victoria  na maeneo mbalimbali ya utawala  ya wilaya  ya Nyamagana. Mkoa  wa Mwanza, upo  pia  kusini  magharibi mwa mkoa wa Mara, mkoa  wa Simiyu na mkoa wa shinyanga
Eneo la kaskazini  la makazi yao ni katika Mbuga  maarufu Serengeti  familia  za wasukuma wengi sana wamehamia  maeneo ya kusini kuelekea  mkoa  wa Rukwa  ambako baadae  umegawanywa  na kuzaa mkoa wa katavi, wakipita  maeneo ya  kabila la  wapimbwe na hivyo kufanya mkazi katika eneo la  kijiji cha wapimbwe.

Shughuli za kiuchumi
Shughuli  kuu za kiuchumi kwa Wasukuma   ni kilimo na uvuvi ufugaji  na  biashara. Pamba ndio zao kuu  la biashara  kwa Wasukuma  ambao pia   hulima  mazao mengine  kama mpunga, tumbaku mahindi, viazi, dengu  na  mahinda  (kisiwani ukerewe) wasukuma  pia  ni wafanyabiashara  na uvivu madini kama vile dhahabu almasi  ma madini ambayo huchimbwa  katika  maeneo mbalimbali mkoa wa Mwanza  na Shinyanga.
Wasukuma  pia wanajihusisha   sana  na kilimo  cha mazao ya nafaka  na mifugo ya aina mbalimbali. Maeneo  ya Shinyanga  wanalima  mazao ya nafaka  kama mahindi  na mpunga  idadi ya watu  ina ongezeka  kwa kasi  na hivyo pia  kuongezaeka  kwa wakulima  na mbogamboga.

Shughuli  za sherehe
Wasukuma  wengi  katika   karne  ya ishirini, walitumia utamaduni wao zaidi katika  kusherehekea  matukio ya nyakati mbalimbali kwa mfano wakati wa mavuno, unyago ndoa  na misiba.  watemi ndio walikuwa viongozi wa  kabila  la wasukuma  na watu walikaa  katika eneo moja.
Dhana ya Fonimu
 Riro, (2012:60) fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho kina uamilifu wa kutofautisha maana kinapochukua nafasi ya kipashio kingine chenye hadhi sawa.
Massamba (2004:12), fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi cha kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake; sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Naye  Mgullu (2012:55) anasema ,fonimu ni kipashio kidogo kabisa  katika lugha  kilicho na uamilifu wa kutofautisha maana katika maneno. Kwa mfano kutoka katika lugha ya kisukuma  unaweza kupata  fonimu zifuatazo;

JEDWALI LINALOONYESHA FONIMU KATIKA LUGHA YA KISUKUMA. (KINASUKUMA - MWANZA)
Fonimu za      Kisukuma
Maana ya Kiswahili

Lekaga…./ l/
 Sekaga …../s/              
Zulaga …../l/
 Zugaga…/g/  
            Enjaga…./Ɉ/
             Engaga…/g/              
Ngubho…/u/
Ngobho…/ɔ/

 acha
  cheka
  vua,
 pika
  chukua,
 ondoka au toka
   kiboko (mnyama)
    mavazi(nguo)




Ø  Kuwepo kwa fonimu /l/ na /s/ katika maneno Lekaga na Sekaga zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Ø  Kuwepo kwa fonimu /l/ na /g/ katika maneno Zulaga na Zugaga zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Ø  Kuwepo kwa fonimu /Ɉ/ na /g/ katika maneno Enjaga na Engaga zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Ø  Kuwepo kwa fonimu /u/ na /ɔ/ katika maneno Ngubho na Ngobho zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Dhana ya Konsonanti katika  lugha  ya Kisukuma.
Massamba  na wenzake  (2004: 27) Konsonanti ni aina  za sauti ambazo hutambulika  kama kuzuia  mkondo wa hewa  utokao mapafuni kupitia  chemba cha kinywa  na chemba ya pua kuondoa nje uzuiaji wa mkondo huo  wa hewa  unaweza  kubana kabisa au kuachia ghafla  kisha kuachia taratibu kama tunatamka  neno  /p/
Naye Masebo (2012:89) Konsonanti ni sauti zinazotamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu mbalimbali hasa kwa kutumia ulimi kama vile /p/, /b/ /d/
Kutokana na fasili hizo, Konsonanti ni sauti za lugha ambazo sauti hizo hewa haiondoki mdomoni moja kwa moja lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.
Katika lugha ya kisukuma tunapata Konsonanti zifuatazo kama zinavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo;-
JEDWALI KUONYESHA KONSONANTI KATIKA LUGHA YA KISUKUMA   (KIMUNASUKUMA- Mwanza)
Konsonanti
Kifonetiki
Neno/ maneno
maana
bh
[β]
Bhabha
Bhose,
Bhochaga
Bhana
Bhanhu

Baba
Wote
 Beba
Watoto
watu
c
 []
Chene
Chagulaga
Chunghu
Hivyo
Chagua
Shimo
d


 [d]
Demaga
Dongo
Duba
Chunga
Chura
Tupa

f                              
[f]
Fulaga
Fulaga
Fungulo
Fua
Puliza
Funguo
ɡ
  (ɡ)
Geshaga
Galukaga
Gojaga
Salimia
Geuka
Ngoja
h
[h]
Hambhohambho
Hatale
Hene?
Humulaga
Afadhali
Pakubwa
Kweli?
nyamaza




j
[Ɉ]
Jaga
jingaga
Jako
Jongaga
Nenda
tongoza
Zako
finya
k
[k]
Keshaga
Kinehe
Kwihebha  (kwigusha)
Kesha
Vipi
kucheza
l
[l]
Lalaga
Lushiko
Lyaga
Lemi
Lala
Siku
Kula
Jua

m
[m]
Minze
Mabhele
Maguta
Mbuli
Maji
Maziwa
Mafuta
mbuzi
n
[n]
Nene
naleho
Nzoka
nsumba
Mimi
Nipo
Nyoka
kijana

p
 [p]
Pelaga
Pungujaga
Pujaga
Kimbia
Punguza
Koboa
s
 [ s]
Sabhuni
Sibhitali
Sebha
sabuni
Hospitali
Mungu
t
[t]
Tolaga
Temaga
Tulaga
Tuja
Kuoa
Kata
Piga
dharau
w
[w]
Walwa
Walaga
Wilaga
Wane
wise

Pombe
Mtoto wa mwisho
Usiku
Wangu
wetu
y
 [j]
Yombo
Yene
Yose
Yunga
kelele
ile
Yote
Chekesha
z
[z]
Zugaga
Zumaleka
Zuma
Pika
Kufariki
Laani
ng’
[ŋ]
Ng’wangaluka
Ng’wanike
Ng’wana
Ng’wadila
Za ahsubuhi
Wasichana
Mtoto
Za jioni
ny
[ɲ]
Nyaga
Nyanda
Nyamu
Upepo
Kijana
paka
sh
[ʃ]
Shilewa
Shitambo
Shikombe
Shijiko
Chakula
Hatua
Kikombe
kijiko







Dhana ya Irabu katika  lugha  ya Kisukuma
 /i/                                                                                    /u/
                                                                                           
/I/                                                                                    /ʊ/

/e/                                                                                     /o/

                                           /a  /
i ii
u uu
ɪ ɪɪ
ʊ ʊʊ
e ee
o oo
a aa







/a/        +irabu
+ kati   
+chini
-mviringo
mfano: abhana- watoto
            Abhizikulu -  wajukuu
Aho – pale    
             
/e/        + irabu
            +mbele
            +nusu chini
 –mviringo
mfano  Bhebhe – wewe
chene –chini
 engaga – toka
/I/         +irabu 
+mbele
–mviringo
     +nusu juu
Ijagi –jagi
Idatu- tatu
Ine-nne
 


/i/         + irabu
+mbele 
-mviringo
+ juu
mfano : ipela – pera
 idoka – duka
idoke-mgomba
 


/ ʊ/             + irabu
+nyuma
+mviringo
+nusu juu

mfano: idatʊ– tatu
 ʊleja - unaenda
ʊlelya – unakula?



      /u/              + irabu 
                         +juu              
                         +nyuma         
                        +mwiringo   
Mfano; mabhu-majivu  
Miundo ya silabi katika lugha ya kisukuma
Riro (2012: 77). silabi ni dhana ya kifonolojia ambayo huwakilisha umbo la matamshi ambapo sauti moja au zaidi hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja la sauti. Ifuatayo ni Miundo ya silabi katika lugha ya kisukuma
        i.            Muundo wa Irabu peke yake  (I)
 mfano: 
                      Ipela – pera
Idatu – tatu
Enzoka – nyoka
Aho – pale
      ii.            Muundo wa Konsonanti + Irabu  (KI)  
mfano: Sekaga  - cheka
Tolaga – oa
Somaga – soma
    iii.            Muundo wa konsonanti + konsonati +Irabu  (KKI)
mfano: 
Embiti – fisi
Ngosha- mwanaume
Chagulaga – chagua
Ntale - mkubwa
Ndoke  - ndizi
    iv.            Muundo wa konsonanti+ kiyeyusho+ Irabu (KI1/2 I)
 mfano:
                        Ulelya - kula
Nyanza – ziwa
      v.            Muundo wa konsonanti peke yake (K)
 mfano:
Mva- mbwa
    vi.            Muundo wa Konsonanti + Konsonanti + kiyegusho + Irabu (KKI1/2 I)

            Mfano;
Nsungwi- sungwi
Ngwala – Ngwara au mtama
DHANA YA ALOFONI  KATIKA  LUGHA  YA KISUKUMA (KINASUKUMA – MWANZA)
Mgullu (2012:59) alofoni ni  sauti mojawapo miongoni mwa sauti kadhaa zinazoiwakilisha fonimu moja. Alofoni hutokea katika mazingira mahususi.
Naye Riro (2012:73) alofoni ni maumbo mawili au zaidi ambayo huakilisha fonimu moja. Waidha alofoni ni matamshi tofauti ya fonimu moja ambayo hujitokeza kutegemea mazingira ya utokeaji ya sauti hiyo.
JEDWALI LIFUATALO LINAONYESHA  ALOFONI KATIKA LUGHA YA KISUKUMA
Kisukuma Mwanza
Kinyantuzu Shinyanga
Kinakiiya Simiyu
Kiswahili
Shikombe
Shitabho
Bhushishi
Shikolo
Shilewa
Sikombe
Sitabho
Bhusisi
Sikolo
Silewa
Jikombe
Jitabho
Bhosisi
Jikolo
Jilewa
Kikombe
kitabu
ukwaju
kitu
chakula

LAHAJA KATIKA LUGHA YA KISUKUMA.
Kamusi  karne ya ishirini  na moja  (2013) lahaja  ni tawi dogo  la lugha  Fulani linalozungumzia  katika  eneo Fulani  la kijiografia lengo tofauti za  kimatamshi kimuundo  matumizi ya maneno kwa mfano; lahaja  ya Kiswahili inayozungumzwa  Mombasa huitwa  kimvita.
Naye Masebo (2012:20) lahaja ni tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza katika lugha kuu yenye asili moja. Tofauti hizo zipo katika matamshi (lafudhi) maumbo au matumizi ya maneno.
Katika lugha ya kisukuma kuna lahaja  kuu tatu  na  lahaja hizo zimegawanyika  kulingana   na  maeneo ya kijiografia  na lahaja  hizo ni kinasukuma, kinyantuzu, kinakiiya.
Lahaja ya Kinasukuma  ni lahaja  ambayo inazungumzwa   na  watu  wa mwanza  na wilaya  zake, kimunasukuma  ni  lahaja   inayojulikana  kama  lahaja ya  kaskazini  ambayo inatumiwa na watu wa  mwanza  na wilaya  zake   kama  vile nyamagana, misungwi sengerema  na ilemela  mfano wa maneno yanayopatikana  katika lahaja  hii ni:-
magulu- miguu
Miso – macho
Nindo – pua
Lahaja ya Kinyantuzu ni lahaja  ya kisukuma  ambayo  inazungumzwa   na watu wa shinyanga  na baadhi ya maeneo ya Simiyu  kama vile bariadi. lahaja  hii  inajulikana  kama lahaja  ya kusini  mfano  wa  maneno  ya lahaja  ya     kinantuzu ni :-
guseka  cheka
sinonu – vitamu
solo- moja
nzwele – nywele
gusula – kufua
mdege – mahindi

Lahaja ya Kinakiiya ni lahaja  ambayo inazungumzwa maeneo ya Simiyu, Bariadi na lamadi, lahaja  hii inajulikana  kama lahaja  ya mashariki, jina  la lahaja hii kinakiiya  limetokana  na  neno la kisukuma ambalo  ni kiiya lenye maana ya mashariki hivyo basi, lahaja hizi tatu zinatofautiana  kwa tofauti za kilekiska na kimfumo
Tofauti za kilekiska.
Hii hutokea pale  ambapo fonimu  iliyochaguliwa   katika neno au maneno kuwa  tofauti katika lahaja   moja  ukilinganisha  na lahaja  nyingine.

Jedwali lifuatalo linaonesha tofauti za kilekiska katika lahaja  za  kisukuma.
Kinasukuma (Mwanza)
Kinyantuzu (Shinyanga)
Kinakiiya (Simiyu)
Kiswahili
Kwigusha
Gwihebha
Kwisinya
Kucheza
Mandege
Mandege
Mdege
Mahindi
wabheja

Obheja

Wabezya
Ahsante
Wawiza

Owiza

Mwiza

Mzuri
Shikolo

Sikolo

Jikolo

Kitu

Tofauti za kimfumo
Katika lugha  ya Kisukuma, kuna baadhi ya lahaja zinakuwa  na sauti /h/  na nyingine zinakuwa hazina sauti hiyo  katika mazingira sawa kwa mfano Kinakiiya  na Kinyantuzu  hazina sauti /h/.



Jedwali lifuatalo linaonyesha tofauti za kimfumo.
Kinasukuma(mwanza)
Kinyantuzu(shinyanga)
Kinakiiya(Simiyu)
Kiswahili
Bhagosha
Bhing’we
Kubhona
Shinonu
Shilewa
Bagosha
Bing’we
Kobona
Sinonu
silewa
Bagosha
Bing’we
Kubona
Jinonu
Jilewa
 Wanaume
Ninyi
Kuona
Vitamu
Chakula

Hitimisho, Kutokana  na utafiti  huu imebainika kabila  la Wasukuma lina wazungumzaji wengi sana  wa lugha  ya kisukuma  katika nchi ya Tanzania mathalani katika  mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita na Simiyu wakati huo wengine  wametawanyika  katika  maeneo  mengine ya Tanzania  kutokana  na mtawanyiko huo shughuli mbalimbali  za  kiuchumi kama vile  kilimo  ufugaji  na uvuvi kama vile  Kinasukuma  kaskazini Mwanza, Kinyantuzu  kusini – Shinyanga, Tabora  na Kinakiiya  Mashariki – Simiyu.


MAREJELEO
 Chubwa, P. (1979). Waha Historia na maendeleo. Tabora: TMP book departiment,
Masebo J. A& Nyangwine N.( 2012). Nadharia ya lugha ya Kiswahili 1:  kidato cha 5&6. Dar    
              es  Salaam Tanzania:  Nyangwine publishers.
Massamba ,D.P.B (2004). Fonolojia ya Kiswahili sanifu(FONIKISA). Dar es salaam: TUKI.
michuzijr.blogspot.com
Mdee na wenzake (2013). kamusi ya karne ya 21. Dar es salaamu Tanzania: Longhorn.
Mgullu, R.S (2011), Mtalaa wa Isimu: Fonetiki , Fonolojia  na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi:  
 Longhorn
Riro, S. M (2012)Dafina ya lugha isimu na nadharia: kwa sekondari, vyuo vya kati na vyuo
            vikuu. Mwanza, Tanzania: Serengeti educational publishers (T) LTD.
ruhuwiko.blogspot.com

9 comments:

  1. Where can I get the English to kinyamwezi dictionary because am trying to find ways of learning my language please... Thanks

    ReplyDelete
  2. Ingefaa kisukuma kifundishwe mashuleni Kama somo

    ReplyDelete
  3. nakupenda kisukuma hadi kesho kutwa na mtondogoo

    ReplyDelete
  4. Neno KONA lina ni nini kwa kisukuma,
    Mf. Amekata KONA hapo mbele

    ReplyDelete
  5. Maana ya kwandu inamaanisha nini

    ReplyDelete
  6. Najifunza kisukuma hii inanisaidia

    ReplyDelete
  7. Your post was both informative and engaging. Much appreciated! Also check the nc gun license

    ReplyDelete