jina
Wasukuma linatokana na neno “sukuma” lenye maana ya “kaskazini” katika lugha ya
Kisukuma na Kinyamwezi. Wanyamwezi waliwaita “Bhasukuma” yaani watu wa
kaskazini mwao. Nao Wasukuma waliwaita Wanyamwezi “Bhadakama”.
Maria
Nyanjige akinukuliwa, asema anafafanua kuhusu historia ya Wasukuma, “
kihistoria asili ya kabila la wasukuma ni nchini Ethiopia, na akaongeza kuwa
kabila la Wasukuma limegawanyika katika sehemu tatu, kwamba kuna wasukuma wa
Mwanza, Wasukuma wa Tabora na Wasukuma wa Shinyanga, akaeleza kuwa pamoja na
kugawanyika kwa makabila hayo lakini bado yanalafudhi inayotofautiana kwa namna
moja ama nyingine” kuna maelezo yahusuyo makumbusho ya Bujora ambapo tamaduni
za Wasukuma zimehifadhiwa. Bujora zamani iliitwa Kujorwaningo kutokana na eneo
hilo kuwa hatari kutokana na wanyama hatari na watu wanyongao watu wengine,
hivyo eneo hilo likabatizwa jina la kujorwaningo yaani kwa kisukuma kunyonga
shingo.
inaelezea
kuwa Kisukuma ni lugha ya kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasukuma mwaka
2006, idadi ya wasemaji wa Kisukuma imehesabiwa kuwa ni watu milioni 543000.
Kufuatana na Uainishaji wa lugha za Kbantu wa Malcom Guthrie, Kisukuma iko
katika kundi la F20. inafanana na lugha ya Kinyamwezi.
Jina “Wasukuma” lina maana ya watu wa “kaskazini” lakini maana hii haiwakilishi
maana halisi ambayo watu wengi
huitafsili kwa mfano Wasukuma hutumia alama
ya utambulisho kwa eneo fulani
kwa viashirio vya makabila kwa mfano jina kama hili: Kiiya
lina maana ya mashariki ambako ni mawio
ya jua. Huu ni utambulisho ambao
haukufanikishwa
ama kuitwa kwa jina la kabila fulani
mfano mwingine ni upande wa
“dakama” ambapo yatambulisha kama eneo la Unyamwezi lakini zaidi ya
mpanuko wake ni upande wa “kusini” zaidi
ya hapo neno hili hutumiwa sana na kabila
la Wanyamwezi ili kutambulisha eneo la Wasukuma ambapo Wasukuma nao husema
“dakama” upande mwingine ambao
unapewa alama ya utambulisho wa neno
“shashi” maana yake ni upande wa kabila la “Washashi”
na neno hili washashi ni mkusanyiko wa makabila
ya mkoa wa Mara.
Japo
pia neno hili “shashi” linamaanisha kabila la Wakurya ambao pia mpanuko wake
unakomea hapo ambapo zaidi ya eneo zima la upande huu unamaanisha upande wa
kaskazini. Upande wa mwisho kutambulishwa
ni “Ngw’eli” neno hili halikupewa
kabla na badala yake linamaanisha
upande mashariki (dira), ambako ni machweo
ya jua. “Wasukuma wenyewe hulirejelea
jina hili kama “bhasukuma” kwa umoja “nsukuma”
Wasukuma
huishi eneo la kaskazini mashariki mwa Tanzania, karibu na
mwambao wa kusini mwa ziwa Victoria
na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya
ya Nyamagana. Mkoa wa Mwanza,
upo pia kusini
magharibi mwa mkoa wa Mara, mkoa
wa Simiyu na mkoa wa shinyanga
Eneo
la kaskazini la makazi yao ni katika
Mbuga maarufu Serengeti familia
za wasukuma wengi sana wamehamia
maeneo ya kusini kuelekea
mkoa wa Rukwa ambako baadae
umegawanywa na kuzaa mkoa wa
katavi, wakipita maeneo ya kabila la
wapimbwe na hivyo kufanya mkazi katika eneo la kijiji cha wapimbwe.
Shughuli za kiuchumi
Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo na uvuvi ufugaji na
biashara. Pamba ndio zao kuu la
biashara kwa Wasukuma ambao pia
hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku mahindi, viazi,
dengu na
mahinda (kisiwani ukerewe)
wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvivu madini kama vile dhahabu almasi ma madini ambayo huchimbwa katika
maeneo mbalimbali mkoa wa Mwanza
na Shinyanga.
Wasukuma pia wanajihusisha sana
na kilimo cha mazao ya
nafaka na mifugo ya aina mbalimbali.
Maeneo ya Shinyanga wanalima
mazao ya nafaka kama mahindi na mpunga
idadi ya watu ina ongezeka kwa kasi
na hivyo pia kuongezaeka kwa wakulima
na mbogamboga.
Shughuli za sherehe
Wasukuma wengi
katika karne ya ishirini, walitumia utamaduni wao zaidi
katika kusherehekea matukio ya nyakati mbalimbali kwa mfano
wakati wa mavuno, unyago ndoa na misiba. watemi ndio walikuwa viongozi wa kabila
la wasukuma na watu walikaa katika eneo moja.
Dhana
ya Fonimu
Riro, (2012:60) fonimu ni kipashio kidogo
kabisa cha lugha ambacho kina uamilifu wa kutofautisha maana kinapochukua
nafasi ya kipashio kingine chenye hadhi sawa.
Massamba
(2004:12), fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha
ambacho kina sifa pambanuzi cha kuweza kukitofautisha na
vipande vingine vya aina yake; sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Naye
Mgullu (2012:55) anasema ,fonimu
ni kipashio kidogo kabisa katika lugha kilicho na uamilifu wa
kutofautisha maana katika maneno. Kwa mfano kutoka katika lugha ya
kisukuma unaweza kupata fonimu
zifuatazo;
JEDWALI
LINALOONYESHA FONIMU KATIKA LUGHA YA KISUKUMA. (KINASUKUMA - MWANZA)
Fonimu za Kisukuma
|
Maana
ya Kiswahili
|
Lekaga…./
l/
Sekaga
…../s/
Zulaga …../l/
Zugaga…/g/
Enjaga…./Ɉ/
Engaga…/g/
Ngubho…/u/
Ngobho…/ɔ/
|
acha
cheka
vua,
pika
chukua,
ondoka au toka
kiboko (mnyama)
mavazi(nguo)
|
|
|
Ø Kuwepo
kwa fonimu /l/ na /s/ katika maneno Lekaga na Sekaga zimepelekea kuwepo kwa
maana tofauti katika maneno hayo.
Ø Kuwepo
kwa fonimu /l/ na /g/ katika maneno Zulaga na Zugaga zimepelekea kuwepo kwa
maana tofauti katika maneno hayo.
Ø Kuwepo
kwa fonimu /Ɉ/ na /g/ katika maneno Enjaga na Engaga zimepelekea kuwepo kwa
maana tofauti katika maneno hayo.
Ø Kuwepo
kwa fonimu /u/ na /ɔ/ katika maneno Ngubho na Ngobho zimepelekea kuwepo kwa
maana tofauti katika maneno hayo.
Dhana ya Konsonanti katika lugha
ya Kisukuma.
Massamba na wenzake
(2004: 27) Konsonanti ni aina za
sauti ambazo hutambulika kama
kuzuia mkondo wa hewa utokao mapafuni kupitia chemba cha kinywa na chemba ya pua kuondoa nje uzuiaji wa
mkondo huo wa hewa unaweza
kubana kabisa au kuachia ghafla
kisha kuachia taratibu kama tunatamka
neno /p/
Naye
Masebo (2012:89) Konsonanti ni sauti zinazotamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa
katika sehemu mbalimbali hasa kwa kutumia ulimi kama vile /p/, /b/ /d/
Kutokana
na fasili hizo, Konsonanti ni sauti za lugha ambazo sauti hizo hewa
haiondoki mdomoni moja kwa moja lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za
pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.
Katika lugha ya
kisukuma tunapata Konsonanti zifuatazo kama zinavyoonyeshwa kwenye jedwali
lifuatalo;-
JEDWALI KUONYESHA KONSONANTI KATIKA
LUGHA YA KISUKUMA (KIMUNASUKUMA-
Mwanza)
Konsonanti
|
Kifonetiki
|
Neno/
maneno
|
maana
|
bh
|
[β]
|
Bhabha
Bhose,
Bhochaga
Bhana
Bhanhu
|
Baba
Wote
Beba
Watoto
watu
|
c
|
[]
|
Chene
Chagulaga
Chunghu
|
Hivyo
Chagua
Shimo
|
d
|
[d]
|
Demaga
Dongo
Duba
|
Chunga
Chura
Tupa
|
f
|
[f]
|
Fulaga
Fulaga
Fungulo
|
Fua
Puliza
Funguo
|
ɡ
|
(ɡ)
|
Geshaga
Galukaga
Gojaga
|
Salimia
Geuka
Ngoja
|
h
|
[h]
|
Hambhohambho
Hatale
Hene?
Humulaga
|
Afadhali
Pakubwa
Kweli?
nyamaza
|
|
|
|
|
j
|
[Ɉ]
|
Jaga
jingaga
Jako
Jongaga
|
Nenda
tongoza
Zako
finya
|
k
|
[k]
|
Keshaga
Kinehe
Kwihebha (kwigusha)
|
Kesha
Vipi
kucheza
|
l
|
[l]
|
Lalaga
Lushiko
Lyaga
Lemi
|
Lala
Siku
Kula
Jua
|
m
|
[m]
|
Minze
Mabhele
Maguta
Mbuli
|
Maji
Maziwa
Mafuta
mbuzi
|
n
|
[n]
|
Nene
naleho
Nzoka
nsumba
|
Mimi
Nipo
Nyoka
kijana
|
p
|
[p]
|
Pelaga
Pungujaga
Pujaga
|
Kimbia
Punguza
Koboa
|
s
|
[ s]
|
Sabhuni
Sibhitali
Sebha
|
sabuni
Hospitali
Mungu
|
t
|
[t]
|
Tolaga
Temaga
Tulaga
Tuja
|
Kuoa
Kata
Piga
dharau
|
w
|
[w]
|
Walwa
Walaga
Wilaga
Wane
wise
|
Pombe
Mtoto wa mwisho
Usiku
Wangu
wetu
|
y
|
[j]
|
Yombo
Yene
Yose
Yunga
|
kelele
ile
Yote
Chekesha
|
z
|
[z]
|
Zugaga
Zumaleka
Zuma
|
Pika
Kufariki
Laani
|
ng’
|
[ŋ]
|
Ng’wangaluka
Ng’wanike
Ng’wana
Ng’wadila
|
Za ahsubuhi
Wasichana
Mtoto
Za jioni
|
ny
|
[ɲ]
|
Nyaga
Nyanda
Nyamu
|
Upepo
Kijana
paka
|
sh
|
[ʃ]
|
Shilewa
Shitambo
Shikombe
Shijiko
|
Chakula
Hatua
Kikombe
kijiko
|
Dhana
ya Irabu katika lugha ya Kisukuma
/i/ /u/
/I/ /ʊ/
/e/ /o/
/a /
i ii
|
|
u uu
|
ɪ ɪɪ
|
|
ʊ ʊʊ
|
e ee
|
|
o oo
|
|
a aa
|
|
|
/a/ +irabu
+
kati
+chini
-mviringo
mfano:
abhana- watoto
Abhizikulu
- wajukuu
Aho
– pale
/e/ + irabu
+mbele
+nusu
chini
–mviringo
mfano Bhebhe – wewe
chene
–chini
engaga – toka
/I/ +irabu
+mbele
–mviringo
+nusu juu
Ijagi
–jagi
Idatu-
tatu
Ine-nne
/i/
+ irabu
+mbele
-mviringo
+
juu
mfano
: ipela – pera
idoka – duka
idoke-mgomba
/
ʊ/ + irabu
+nyuma
+mviringo
+nusu juu
mfano:
idatʊ– tatu
ʊleja - unaenda
ʊlelya
– unakula?
/u/
+ irabu
+juu
+nyuma
+mwiringo
Mfano;
mabhu-majivu
Miundo ya silabi katika lugha ya
kisukuma
Riro
(2012: 77). silabi ni dhana ya kifonolojia ambayo huwakilisha umbo la matamshi
ambapo sauti moja au zaidi hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja la sauti. Ifuatayo
ni Miundo ya silabi katika lugha ya kisukuma
i.
Muundo
wa Irabu peke yake (I)
mfano:
Ipela – pera
Idatu – tatu
Enzoka – nyoka
Aho – pale
ii.
Muundo
wa Konsonanti + Irabu (KI)
mfano:
Sekaga - cheka
Tolaga – oa
Somaga – soma
iii.
Muundo
wa konsonanti + konsonati +Irabu (KKI)
mfano:
Embiti – fisi
Ngosha- mwanaume
Chagulaga – chagua
Ntale - mkubwa
Ndoke - ndizi
iv.
Muundo
wa konsonanti+ kiyeyusho+ Irabu (KI1/2 I)
mfano:
Ulelya
- kula
Nyanza – ziwa
v.
Muundo
wa konsonanti peke yake (K)
mfano:
Mva- mbwa
vi.
Muundo
wa Konsonanti + Konsonanti + kiyegusho + Irabu (KKI1/2 I)
Mfano;
Nsungwi- sungwi
Ngwala – Ngwara au
mtama
DHANA
YA ALOFONI KATIKA LUGHA
YA KISUKUMA (KINASUKUMA – MWANZA)
Mgullu (2012:59)
alofoni ni sauti mojawapo miongoni mwa sauti kadhaa zinazoiwakilisha
fonimu moja. Alofoni hutokea katika mazingira mahususi.
Naye Riro (2012:73)
alofoni ni maumbo mawili au zaidi ambayo huakilisha fonimu moja. Waidha alofoni
ni matamshi tofauti ya fonimu moja ambayo hujitokeza kutegemea mazingira ya
utokeaji ya sauti hiyo.
JEDWALI
LIFUATALO LINAONYESHA ALOFONI KATIKA
LUGHA YA KISUKUMA
Kisukuma
Mwanza
|
Kinyantuzu
Shinyanga
|
Kinakiiya
Simiyu
|
Kiswahili
|
Shikombe
Shitabho
Bhushishi
Shikolo
Shilewa
|
Sikombe
Sitabho
Bhusisi
Sikolo
Silewa
|
Jikombe
Jitabho
Bhosisi
Jikolo
Jilewa
|
Kikombe
kitabu
ukwaju
kitu
chakula
|
LAHAJA
KATIKA LUGHA YA KISUKUMA.
Kamusi karne ya ishirini na moja
(2013) lahaja ni tawi dogo la lugha
Fulani linalozungumzia
katika eneo Fulani la kijiografia lengo tofauti za kimatamshi kimuundo matumizi ya maneno kwa mfano; lahaja ya Kiswahili inayozungumzwa Mombasa huitwa kimvita.
Naye
Masebo (2012:20) lahaja ni tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza katika lugha kuu
yenye asili moja. Tofauti hizo zipo katika matamshi (lafudhi) maumbo au
matumizi ya maneno.
Katika
lugha ya kisukuma kuna lahaja kuu tatu na
lahaja hizo zimegawanyika
kulingana na maeneo ya kijiografia na lahaja
hizo ni kinasukuma, kinyantuzu,
kinakiiya.
Lahaja ya Kinasukuma ni lahaja
ambayo inazungumzwa na watu
wa mwanza na wilaya zake, kimunasukuma ni
lahaja inayojulikana kama
lahaja ya kaskazini ambayo inatumiwa na watu wa mwanza
na wilaya zake kama
vile nyamagana, misungwi sengerema
na ilemela mfano wa maneno
yanayopatikana katika lahaja hii ni:-
magulu-
miguu
Miso
– macho
Nindo
– pua
Lahaja ya Kinyantuzu ni
lahaja ya kisukuma ambayo
inazungumzwa na watu wa shinyanga na baadhi ya maeneo ya Simiyu kama vile bariadi. lahaja hii
inajulikana kama lahaja ya kusini
mfano wa maneno
ya lahaja ya kinantuzu ni :-
guseka cheka
sinonu
– vitamu
solo-
moja
nzwele
– nywele
gusula
– kufua
mdege
– mahindi
Lahaja ya Kinakiiya
ni lahaja ambayo inazungumzwa maeneo ya Simiyu,
Bariadi na lamadi, lahaja hii
inajulikana kama lahaja ya mashariki, jina la lahaja hii kinakiiya limetokana
na neno la kisukuma ambalo ni kiiya lenye maana ya mashariki hivyo basi,
lahaja hizi tatu zinatofautiana kwa
tofauti za kilekiska na kimfumo
Tofauti za kilekiska.
Hii
hutokea pale ambapo fonimu iliyochaguliwa katika neno au maneno kuwa tofauti katika lahaja moja
ukilinganisha na lahaja nyingine.
Jedwali
lifuatalo linaonesha tofauti za kilekiska katika lahaja za
kisukuma.
Kinasukuma
(Mwanza)
|
Kinyantuzu
(Shinyanga)
|
Kinakiiya
(Simiyu)
|
Kiswahili
|
Kwigusha
|
Gwihebha
|
Kwisinya
|
Kucheza
|
Mandege
|
Mandege
|
Mdege
|
Mahindi
|
wabheja
|
Obheja
|
Wabezya
|
Ahsante
|
Wawiza
|
Owiza
|
Mwiza
|
Mzuri
|
Shikolo
|
Sikolo
|
Jikolo
|
Kitu
|
Tofauti za kimfumo
Katika
lugha ya Kisukuma, kuna baadhi ya lahaja
zinakuwa na sauti /h/ na nyingine zinakuwa hazina sauti hiyo katika mazingira sawa kwa mfano Kinakiiya na Kinyantuzu
hazina sauti /h/.
Jedwali
lifuatalo linaonyesha tofauti za kimfumo.
Kinasukuma(mwanza)
|
Kinyantuzu(shinyanga)
|
Kinakiiya(Simiyu)
|
Kiswahili
|
Bhagosha
Bhing’we
Kubhona
Shinonu
Shilewa
|
Bagosha
Bing’we
Kobona
Sinonu
silewa
|
Bagosha
Bing’we
Kubona
Jinonu
Jilewa
|
Wanaume
Ninyi
Kuona
Vitamu
Chakula
|
Hitimisho,
Kutokana na utafiti huu imebainika kabila la Wasukuma lina wazungumzaji wengi sana wa lugha
ya kisukuma katika nchi ya Tanzania
mathalani katika mikoa ya Mwanza,
Shinyanga, Geita na Simiyu wakati huo wengine
wametawanyika katika maeneo
mengine ya Tanzania kutokana na mtawanyiko huo shughuli mbalimbali za
kiuchumi kama vile kilimo ufugaji
na uvuvi kama vile
Kinasukuma kaskazini Mwanza, Kinyantuzu kusini – Shinyanga, Tabora na Kinakiiya
Mashariki – Simiyu.
MAREJELEO
Chubwa, P.
(1979). Waha Historia na maendeleo. Tabora: TMP book
departiment,
Masebo
J. A& Nyangwine N.( 2012). Nadharia
ya lugha ya Kiswahili 1: kidato cha
5&6. Dar
es Salaam Tanzania: Nyangwine publishers.
Massamba ,D.P.B (2004). Fonolojia ya Kiswahili
sanifu(FONIKISA). Dar es salaam:
TUKI.
michuzijr.blogspot.com
Mdee
na wenzake (2013). kamusi ya karne ya 21.
Dar es salaamu Tanzania: Longhorn.
Mgullu, R.S (2011), Mtalaa wa Isimu: Fonetiki , Fonolojia
na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi:
Longhorn
Riro, S. M (2012)Dafina ya lugha isimu na
nadharia: kwa sekondari, vyuo vya kati na vyuo
vikuu. Mwanza, Tanzania: Serengeti educational publishers (T) LTD.
ruhuwiko.blogspot.com